Ingia / Jisajili

Usifiwe Moyo Wa Yesu

Mtunzi: S. Mutaboyerwa
> Tazama Nyimbo nyingine za S. Mutaboyerwa

Makundi Nyimbo: Moyo Mtakatifu wa Yesu

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 1,565 | Umetazamwa mara 4,306

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

(Usifiwe Moyo wa Yesu, utukuzwe moyo wa Yesu, utukuzwe na watu wote, tena utukuzwe mahali pote) - Tenor & Bass

Moyo mtukufu wa Yesu kweli umejaa mapendo
Moyo wenye huruma nyingi sada yetu wakosefu
Utukuzwe Moyo wa Yesu uliotuletea wokovu.

  1. Moyo wenye mapendo kwetu, mapendo yasiyo kifani, uliojitoa sadaka kwa ajili yetu sote ushangiliwe kwa furaha kubwa popote duniani.
     
  2. Sipati maneno yenye kufaa kueleza moyo huo, niende wapi niazime maneno yatakayonifaa kueleza sifa za moyo huo uliompendeza Baba, moyo wenye utii, uliotii mpaka kufa.
     
  3. Ewe Mungu Baba Mwenyezi utuhurumie wanao, ee Mungu Baba mwenyezi utuhurumie wanao kwa ajili ya Moyo huu Mtakatifu wa Yesu. Tazameni heshima yake na malipizi ee Baba utujalie fanaka utupe Baraka zako.

HITIMISHO (Baada ya Shairi la 3)

Siku zote nitakusifu kwa ibada na nyimbo nzuri, nitatuza moyo huu uliotuletea wokovu usifiwe uabudiwe Moyo uliojaa mapendo.


Maoni - Toa Maoni

May 09, 2016
Saafi kabisa

Toa Maoni yako hapa