Utukufu Wa Msalaba
Utukufu wa msalaba, twaadhimu twauabudu, twaomba utukomboe Bwana sisi tuwakosefu.
Utukufu wa msalaba, twaadhimu twausujudu, twaomba utukomboe.
1. Kwa ishara ya msalaba, twautukuza msalaba, wenye ushindi na uzima.
2. Katika msalaba wako, uliteswa kwa dhambi zetu, twaomba utuhurumie.
3. Katika msalaba wako, twapata msamaha wako, twaomba utuhurumie.
4. Na msihofu kitu kamwe, tazama msalaba wake, mpate ujasiri.
5. Njoni enyi msumbukao, na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
6. Chini ya msalaba wako, twapata utulivu wa roho, na tabasamu ya heri.