Ingia / Jisajili

Wapendwa Familia Ya Mungu

Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama

Makundi Nyimbo: Anthem

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 551 | Umetazamwa mara 2,566

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

WAPENDWA FAMILIA YA MUNGU

//:Wapendwa familia ya Mungu tunawatakia salamu za upendo, salamu za amani na matashi mema; ziwe kwenu nyote, ziwe kwenu nyote://

Ikumbukwe kwamba sisi wana Mwanza tulizindua rasmi ujenzi wa kanisa, kanisa kuu la jimbo letu mwezi wa kumi mwaka elfu mbili na kumi na mbili; Hivyo wapendwa wanajimbo wote tutambue kwamba kazi hii nzito inayohitaji mshikamano wetu, ushirikiano na ukarimu wetu wanajimbo kuu la Mwamza;

Tunahimizwa wanajimbo wote kushiriki ujenzi huu, ujenzi wa kanisa la Jimbo Kuu, Jimbo la Mwanza.

//:Tutumie uwezo aliotujalia Mungu - Tutumie uwezo, uwezo wa hali na mali, tutumie uwezo wetu wote aliptujalia Mungu://

Tunatambua uongozi imara, uongozi wa Baba Askofu Thadeus Ruwai'ch; aliuzindua kwa ibada ya misa takatifu, eneo likapimwa na ramani ikatolewa; hiyo ni hatua kubwa, ni hatua ya kuungwa mkono.

Enyi wapendwa familia ya Mungu tukumbuke kuongozwa na sala na kazi na matoleo yetu kwa kanisa Katoliki.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa