Mtunzi: Gasper Tesha
> Tazama Nyimbo nyingine za Gasper Tesha
Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Pasaka
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 1,222 | Umetazamwa mara 4,412
Download Nota Download MidiNitamwimbia Bwana nitamwimbia Bwana kwa maana ametukuka na kwa maana ametukuka sana. Farasi na mpanda farasi wote amewatupa baharini ni kwa maana ametukuka sana, farasi na mpanda farasi wote amewatupa baharini.
1. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu naye amekuwa wokovu wangu yeye ni Mungu wangu na mimi nitamsifu yeye milele ni Mungu wa Baba yangu na mimi nitamtukuza yeye milele
2. Bwana yeye ni mtu wa vita Bwana hilo ndilo jina lake magari ya Farao na jeshi lalke amewatupa wote baharini vilindi vya maji vimewafunika walizama ka majiwe
3. Bwana mkono wako wa kuume umepata fahari na uwezo Bwana mkono wako wa kuume unawasetaseta adui kwa wingi wa huo ukuu wako wawaangusha chini adui zako
4. Utawaingiza na kuwapanda katika mlima wa urithi wako mahali pale ulipojifanyia Ee Bwana ili upate kukaa patakatifu palipo imara Bwana atatawala milele