Ingia / Jisajili

Wimbo Wa Taifa Wa Tanzania (Tanzania National Anthem)

Mtunzi: Enoch Sontonga

Makundi Nyimbo: Anthem

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 24,554 | Umetazamwa mara 67,970

Download Nota
Maneno ya wimbo

Mungu ibariki Afrika

Wabariki viongozi wake

Hekima umoja na amani

Hizi ni ngao zetu

Afrika na watu wake

Ibariki  Afrika

Ibariki  Afrika

Tubariki watoto wa Afrika

Mungu ibariki Tanzania

Dumisha uhuru na umoja

Wake kwa waume na watoto

Mungu ibariki

Tanzania na watu wake

Ibariki Tanzania

Ibariki Tanzania

Tubariki watoto wa Tanzania


Maoni - Toa Maoni

Kingi Sep 15, 2021
Natoa pongezi kwa mtunzi wa wimbo wetu wa taifa lakini pia pongezi kwa aliyeuweka wimbo huu kwenye swahili notes (Ukweli ni kwamba mtunzi wa wimbo wetu ni Enoch sontoga kwa lugha ya kizuru yani (Nkosi sikelel i Africa ) ulitumika hata kwenye vuguvugu la umajumui ya Africa kwa Africa hivyo basi melody na harmony ni ya ndugu SONTOGA lakini kwa lugha ni watanzania waliotumia kiswahili pia ukifatilia vizuri melody hii utaikuta Zimbabwe,Namibia na Zambia na South Africa inatumika lakini kwenyewe wimbo una sehemu kuu tatu 1kizuru,kiafricanaas na kingereza .hivyo basi tukubali kazi za wenzetu

Mongassa Oct 05, 2019
Asili ya Melody ya wimbo huu siyo South Africa National Anthem,wimbo huu asili yake Tanzania na mtunzi ni Mtanzania na siyo aliweka maneno tu.Ikumbukwe kuwa Tanzania imepata Uhuru kabla ya South Africa,kwenye harakati za ukombozi kusini mwa jangwa la Sahara Tanzania imeshiriki kwa asilimia kubwa na moja ya mambo iliyosaidia ni pamoja na kuiruhusu South Africa kuitumia Nyimbo ya Taifa la Tanzania,na ikumbukwe pia siyo wao tu hata Zambia walipewa ruhusa hiyo(ukipata muda tafuta wimbo wa taifa wa Zambia) Zambia pia waliweka maneno tu na tofauti yetu na wao ni Lugha,nyakati kaburu kashika hatamu South Africa haikuruhusiwa kutunga,kuimba,ama kusaambaza jumbe za aina hii.NADHANI IFIKE MAHALI TUHESHIMU NA KUENZI KAZI ZETU.Aliye nakili wimbo huu anapaswa kuhariri eneo hili,kwani ni kinyume cha hapo ni kosa kisheria,hata kuurekebisha wimbo huu unapaswa kupata kibali,kuusambaza pia unapaswa kupata kibali,Wimbo huu ni moja ya tunu za Taifa,sina uhakika kama ile sheria inaitwa makosa yakimtandao kama inafanya kazi,!wahusika Wakifuatilia hata tovuti hii inakuwa kwenye wakati mgumu,kuruhusu nakusambaza kazi hii tena pakiwa na makosa kama haya. MAONI YANGU. Wimbo huu ni mkubwa kuliko tunavyoufikiria,ADMIN toa wimbo huu na uhakikiwe haraka na kuuweka tena lazima ufuate kibali toka kwa mamlaka husika.Ikumbukwe tovuti inasomwa Dunia nzima,inaingia akilini walioanza kuutumia tokea miaka ya sitini waje wakopi kwa aliyeanza kuutumia mwaka 1994? Kabla yakufanya jambo tupende hata kufuatilka mambo. Mungu na atupe neema ya Ufahamu. AMINA.

Paschal Faustni Mwekundu Dec 04, 2018
Ha

juma tabu damiao Nov 09, 2018
PONGEZI KWA MTUNZI WA MASHAILI YALIYOTUMIKA KUUNDA WIMBO WA TAIFA LETU LA TANZANI. MUNGU AMBALIKI POPOTE PALE ALIPO KWA KUTUNGA WIMBO MZULI NA WAKUPENDEZA. AISEEE NAUPENDA SANA WIMBO HUU UNAPOKUWA UKIIMBWA HASA NAMIMI NIKIWA MIONGONI MWAO WAIMBAJI NAJISIKIA FULAHA TELE. GOD BLESS IN TANZANIA. PAMOJA NA WATU PIA MKUMBUSHE ANKO MAGU KUWA KGM BILA ZIWA TANGANYIKA NI FULL MAJANGA HIVYO AJALIBU KUBANA NA KULEGEZA ILI WATU TUPATE KUSOGEZA SIKU MBELE KGD. NI MTANZANIA MWENYE ASILI YA DRC

YUSUPH IDDI MGANDA Aug 20, 2018
Napenda kumpa pongezi kubwa sana mtunzi wa nyimbo ya taifa naisi kipindi alitunga nyimbo iyo alikua hana isia kubwa na taifalake tena sana yapaswa apewe zawadi kubwa sana ju ya utunzi wake mungu baliki tanzania mungu m.baliki na mwimbaji hamen

Joseph Thomas Aug 04, 2018
nampongeza Sana aliyeweka wimbo huu kwani nilikuwa nazitafuta sana nota make.asante sana.

Josephath Elias Jun 05, 2018
Pongeza, Kosoa.... Uwe mstaarabu

Abdussamiy Mbuvi Mar 28, 2018
Mie ni Mkenya ila naupenda sana wimbo huu, maana nauona kama wa Africa nzima, Naipenda Kenya, Naipenda Tanzania na Afrika kwa jumla, napenda pia "Tazama ramani..."

projenus Jan 10, 2018
wimbo huu uelimishwe kwa kila mtanzania maana wap watanzania awajui hata mstar mmoja

Gaspeer Jan 02, 2018
Kazi nzuri. Heshima kwa wimbo huu.

Maghen Juma Nov 29, 2017
NAIPENDA TANZANIA NCHI YANGU

Frank Ochumba Nov 22, 2017
naupenda sana wimbo wa taifa, mungu ambariki sana alietunga wimbo huo, #tanzania_kwanza

Wille mecky Nov 13, 2017
Napenda nyimbo ya taifa kama navyo penda nch yangu

Adamu misilwa silole Oct 29, 2017
nimejifunza hutoka kwenu nashukuru sana

John Aug 12, 2017
napenda wimbo wataifa retu raaman nanastiza vijana wenzangu waupende naheshimu

Mukoya Aywah Jun 11, 2017
Mashallah! Napendezwa sana na wimbo huu.Naomba kupata kanda.

Edwine Piuce Mar 26, 2017
Wimbo huu una maana kubwa inabidi uheshimiwe na kila mtu kwa manugaa ya taifa!

Daniel Feb 02, 2017
Nimependa kupta nyimbo hii y taifa tupeni nyimbo zingine

Paschal Edward Rweumbiza Jan 13, 2017
Mungu ibariki tanzania,yaani wimbo huu unatakiwa uheshimiwe,tuwafundishe vijana wetu maana ya nyimbo za mataifa zina maana gain.maana vijana wanafananisha wimbo huu na Mziki Wa kawaida tu,hata ukiimbwa hakuna anayeshtuka.Linganisha walioutazama na waliotazama Salome wimbo Wa juzi utaona kuwa hawana habari nao.tubadilike watanzania.

Paschal Edward Rweumbiza Jan 13, 2017
Mungu ibariki tanzania,yaani wimbo huu unatakiwa uheshimiwe,tuwafundishe vijana wetu maana ya nyimbo za mataifa zina maana gain.maana vijana wanafananisha wimbo huu na Mziki Wa kawaida tu,hata ukiimbwa hakuna anayeshtuka.Linganisha walioutazama na waliotazama Salome wimbo Wa juzi utaona kuwa hawana habari nao.tubadilike watanzania.

Paschal Edward Rweumbiza Jan 13, 2017
Mungu ibariki tanzania,yaani wimbo huu unatakiwa uheshimiwe,tuwafundishe vijana wetu maana ya nyimbo za mataifa zina maana gain.maana vijana wanafananisha wimbo huu na Mziki Wa kawaida tu,hata ukiimbwa hakuna anayeshtuka.Linganisha walioutazama na waliotazama Salome wimbo Wa juzi utaona kuwa hawana habari nao.tubadilike watanzania.

Adam Marley Dec 21, 2016
Nmependa kupata hizi notes ila naomba wekeni nyimbo nyingi zaidi tujifunzze

Buruhani ngonyani Oct 05, 2016
Naomba mungu aendelee kutulindia amani tuliyonayo, maana tanzania yetu ndio nchi ya furaha.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Ally Hamisi Jun 16, 2016
Pongeza, Kosoa.... Uwe mstaarabu Naupenda sana wimbo wa taifa kwa moyo wangu wote na ninawashauri wananchi wa jamhuri ya muungano wa tanzania tuuheshimu wimbo wa taifa kwa ustaarabu

Daudi Jun 15, 2016
Nimeupenda

Albano John Ammuly May 30, 2016
Naupenda Sana Wimbo Wa Taifa Nawaomba WATANZANIA Wenzangu Tuuweshim Wimbo Wetu Maad Utakuta Adi Vilabuni Walevi Wanaimba Imba Ovyo Bila Utaratitibu

Toa Maoni yako hapa