Ingia / Jisajili

Yesu Anamponya Kipofu

Mtunzi: Fidelis. Kashumba
> Tazama Nyimbo nyingine za Fidelis. Kashumba

Makundi Nyimbo: Anthem | Mafundisho / Tafakari | Tenzi za Kiswahili

Umepakiwa na: Lawrence Nyansago

Umepakuliwa mara 1,938 | Umetazamwa mara 5,964

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

YESU ANAMPONYA KIPOFU

Wakati Yesu alipokuwa (Yeriko) kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba, aliposikia umati (wa watu) ukipita aliuliza kuna nini? wakamwambia Yesu wa Nazareti anapita hapa naye akapaza sauti Yesu mwana wa Daudi unihurumie wale wote waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze lakini yeye akazidi kupaza sauti Mwana wa Daudi nionee huruma. Yesu alisimama akaamuru wamlete kwake yule kipofu alipokuja karibu Yesu akamuuliza unataka nikufanyie nini naye akamjibu Bwana ninaomba nipate kuona tena. Yesu akamwambia ona imani yako imekuponya, na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona akamfuata Yesu akamtukuza Mungu wale watu wote walioona hayo wakamsifu Mungu wakamsifu Mungu wakamsifu Mungu wakamsifu Mungu wakamsifu Mungu wakamsifu Mungu.


Maoni - Toa Maoni

Cosmas Ondieki Abuya Nov 06, 2018
Pongeza.

Toa Maoni yako hapa