Ingia / Jisajili

Yesu Wangu Mpenzi

Mtunzi: Fr. Malema. L. Mwanampepo
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Malema. L. Mwanampepo

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 23,560 | Umetazamwa mara 34,925

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
  1. Yesu wangu mpenzi nakutamani we, uje moyoni mwangu, unitie nguvu za kukupenda 

    Pokea moyo wangu ee Mungu wangu, niweze kukupenda kwa pendo lako

    (Unipe moyo wako ewe Yesu mkombozi wangu shinda mwangu nami daima mwako) x2

  2. Njoni waamini tumwabudu Yesu, chini ya maumbo haya ya mkate mtakatifu na divai
  3. Shida za roho ni pia na za mwili, zote kwa kutolea, tupate kukupenda siku zote
  4. Karamu ya roho Yesu atulisha, kwa moyo safi twende, kula mwili wake kunywa damuye
  5. Kukaa na Yesu duniani hapa, ni heri na faraja, katika mateso umwite Yesu
  6. Ee mana wa mbingu ushibishe roho, jaza mema moyoni, Ee mkombozi Yesu uzima wangu
  7. Ee Yesu njoo Mungu afike upesi usiniache, peke saa ya mwisho Yesu mwema


Maoni - Toa Maoni

Sylvesta chilewa Jul 21, 2018
Ni wimbo mzr

fidelis alcard Aug 19, 2016
upo vizuri but naomba kusaidiwa kukua kimziki

Toa Maoni yako hapa