Ingia / Jisajili

Zitafakarini Njia Zenu

Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 1,064 | Umetazamwa mara 3,068

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

ZITAFAKARINI NJIA ZENU

//:Zitafakarini njia zenu enyi watu wangu://
//: Pandeni milimani mkalete miti, mkaijenge nyumba yangu, nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa://

1. Fikirini kama mnafanya vema enyi watu wangu, ninyi mwakaa kwenye majumba yenu, majumba ya kifahari, lakini mimi Mungu mwumba wenu mmeniacha kwenye magofu.

2. Mnakula bali hamshibi na kunywa lakini hamtosheki, mnavaa lakini hamsikii, hamsikii joto, mishahara yenu inatoweka kama imewekwa mifuko ya kutoboka.

3. Sasa iweni imara enyi watu wote katika nchi, fanyeni kazi kwa kuwa mimi nipo, mimi nipo nanyi, ndilo agano kati yangu nanyi nilipowatoa kule Misri.


Maoni - Toa Maoni

Peter Leonard Oct 01, 2016
Hongera kwa kutunga wimbo huu. Ni mzuri sana. Nimeupenda sana. Mungu akubariki sana.

Toa Maoni yako hapa