Ingia / Jisajili

Ahadi

Mtunzi: Mwita Isack
> Tazama Nyimbo nyingine za Mwita Isack

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mwita Isack

Umepakuliwa mara 2,745 | Umetazamwa mara 2,916

Download Nota
Maneno ya wimbo
UTANGULIZI. (Yupo yule aliyeahidi) ataniwekea makao mbinguni (Naye ndiye Yesu Kristo) aliye niahidi, (Nayo ni hamu ya moyo wangu) kuuona uso wa Bwana wangu (Nikamlaki mawinguni) nikafurahi naye. KIITIKIO. Niliyafungua macho yangu,na nikatazama,ili nimuone ashukapo toka mawinguni, Maana aliniahidi kuwa,atarudi tena,kunichukua nikafurahi pamoja mbinguni,ni hamu ya kila mmoja,kuingia kule mbinguni,tukafurahi na Mwokozi,milele mbinguni x2 SHAIRI. (1) Na akaniahidi Bwana,magumu nikivumilia,nitamuona mbinguni,kwenye kiti cha enzi. (2) Moyo wangu umetulia,umetulia kabisa,kwa kuwa najua ya kwamba,ninalo tumaini. HITIMISHO. (Ni kipi kitanizuia,nisiuone,uso wa Bwana) hakuna (Si kwamba nimekwishafika,bali nipo nakaza mwendo) nifike,(kule mbinguni kwa Baba) nifike mbinguni kwa Baba,nikafurahi na watakatifu,mbinguni (huko Mwokozi aliko) nifike mbinguni kwa Baba,nikafurahi na watakatifu,mbinguni (ni matamanio yangu) nifike mbinguni kwa Baba,nikafurahi na watakatifu,mbinguni (hivyo ninakaza mwendo) nifike mbinguni kwa Baba,nikafurahi na watakatifu,mbinguni (Bwana uniongoze) nifike mbinguni kwa Baba,nikafurahi na watakatifu,mbinguni (kwako nikufikie) nifike mbinguni kwa Baba,nikafurahi na watakatifu,mbinguni.

Maoni - Toa Maoni

Finias Mkulia Aug 18, 2024
Naomba kopi ya wewe Bwana ndiwe mtakatifu wa Mungu

Toa Maoni yako hapa