Mtunzi: Victor Murishiwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Victor Murishiwa
Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 4,546 | Umetazamwa mara 8,139
Download Nota Download Midi{ Ee Mungu Mungu wangu (moyo)
Moyo wangu u thabiti (thabiti)
Nitaimba nitaimba, nitaimba zaburi
{ Amka kinanda ewe kinanda - amka ewe kinanda
Amka kinubi ewe kinubi - amka ewe kinubi
Nitaamka alfaji-ri nitamuimbia Bwana. } *2
1. Ee Mungu nitakushukuru kati ya watu
Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa
2. Kwa maana fadhili zako ni za milele
Na uaminifu wako hata juu mawinguni
3. Ee Mungu utukuzwe juu ya mbingu yote
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako