Ingia / Jisajili

Asante Muumba

Mtunzi: Mike E. Achacha
> Mfahamu Zaidi Mike E. Achacha
> Tazama Nyimbo nyingine za Mike E. Achacha

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Mike Edwin

Umepakuliwa mara 55 | Umetazamwa mara 91

Download Nota
Maneno ya wimbo
ASANTE MUUMBA. 1.Njoni watu wote tucheze mbele za bwana, njoni na vinanda zeze hata vinumbi, ni siku ya furaha, na tuifanye shangwe, Mungu anatupenda twasema ni asante. Asante Baba mwenyezi Mungu muumba wa vyote, umekuwa mwema kwetu Bwana tunashukuru, (kuimba tunaimba, kucheza tunacheza, makofi tunapiga, kuruka tunaruka kwa shukrani.) X2 2.Tazama ndege wa angani wanavyoruka, hata wanyama wa porini wanaruka, wakimsifu Mungu , kwa upendo wake, nawe ujiulize kwa nini usishukuru. 3.Tunakushukuru ee Mungu kwa nyimbo, upendo wako kwetu baba ni wa ajabu, ee Mungu tunashukuru, kwa uhai umetupa, kutupenda bila mwisho twasema ni asante. @Michael E. Achacha

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa