Ingia / Jisajili

Atukuzwe Bwana

Mtunzi: Augustine Rutakolezibwa
> Mfahamu Zaidi Augustine Rutakolezibwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Augustine Rutakolezibwa

Makundi Nyimbo: Anthem | Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: AUGUSTINE RUTAKOLZIBWA

Umepakuliwa mara 1,133 | Umetazamwa mara 4,629

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Atukuzwe Bwana Bwana Mungu wa Israeli x2

Kwakuwa kwakuwa atawajia watu wake na kuwa komboa x2

Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi mtumishi wake

Kama alivyosema kama alivyosema alivyosema tangu mwanzo

Kwa kinywa cha manabii wako watakatifu x2

Tuokolewe na adui zetu na mikononi (mwao wote) wanaotuchukia ilikuwa tendea rehema baba zetu agano takatifu kwa kiapo alichomwapia Ibrahimu Baba yetu x2

Ya kwamba atatujilia sisi tuokoke mikononi mwa adui zetu nakumwabudu pasipo hofu

Kwa utakatifu na kwa haki mbele zako siku zetu zote

Nawe mtoto utaitwa nabii wake aliye juu aliye juu

Kwa maana utatangulia mbele ya uso wa Bwana umtengenezee njia zake njia zake x2

Uwajulishe watu watu wake wokovu katika kusamehewa dhambi zao kwa njia ya rehema za Mungu wetu ambazo kwa hizo mwangaza umetufikia utokao juu

Kawaangaza wakao katika giza na uvuli wa mauti na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa