Mtunzi: C. Mzena
> Tazama Nyimbo nyingine za C. Mzena
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 1,785 | Umetazamwa mara 4,913
Download Nota Download MidiBwana Ameufunua wokovu wake machoni pamataifa amedhihirisha haki yake x2;
Mashairi.
1 (a) Mwimbieni Bwana wimbo mpya,kwa maana ametenda mambo ya ajabu
(b) Mkono wa kuume wake Bwana mkono wake umemtendea ya wokovu
2 (a) Ameukumbuka wema wake na uaminifu kwa nyumba ya Israeli
(b) Miisho yote ya ulimwengu imeuona wokovu wa Mungu wetu
3 (a) Mshangilieni Bwana Mungu furahini enyi nchi zote za dunia
(b) Mwimbieni Bwana kwa kinubi tarumbeta pia mvumo wa baragumu