Ingia / Jisajili

Roho Mtakatifu Tuimarishe

Mtunzi: C. Mzena
> Tazama Nyimbo nyingine za C. Mzena

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Pentekoste

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 320 | Umetazamwa mara 1,104

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ewe Roho Mtakatifu mwalimu wetu Amini, Ni wewe Roho wa hekima na mafunuo ya kweli, uwaangaze waimarishe watumishi wa kanisa waliongoze vema taifa hili la Mungu x 2.

Mashairi:

1. Wanayo kazi yakufundisha na kutakasa Taifa lako, Wanahitaji hekima yako iwaongoze watende vema, Ewe Roho Mtakatifu.

2. Wametwaliwa kati ya watu kwa ajili ya wokovu wetu, Wafanye kazi ya kuchunga Taifa la Mungu ndiyo kanisa, Ewe Roho Mtakatifu.

3. Magumu mengi wanapitia pia changamoto za maisha, Waepushie vikwazo vyote na mitego yake ibilisi, Uwatakase Ee Bwana


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa