Ingia / Jisajili

Bwana Anakuja (Karibu Bwana Njoo)

Mtunzi: Fr. B. Songoro
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. B. Songoro

Makundi Nyimbo: Majilio

Umepakiwa na: Eusebius Joseph Mikongoti

Umepakuliwa mara 11,090 | Umetazamwa mara 17,816

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

BWANA ANAKUJA (KARIBU BWANA NJOO) - Fr. B. Songoro

1. Bwana anakuja twendeni kumlaki, Bwana Mungu wa majeshi

    Ziwasheni nyoyo tukampokee huyu mwenye utukufu.

Kiitikio:

Karibu Bwana njoo, Karibu Bwana njoo; shinda pamoja nasi x 2.

2. Wewe ndiwe mkate, mkate wa Mbinguni, utulishe wenye njaa
    Wewe ndiwe mwanga, sisi tu vipofu, tufanye tuone tena.
 
3. Wewe ndiwe njia, tutakufuata, turudi kwa Baba yetu
    Wewe ni ukweli utuangazie, tusije tukapotoka.
 
4. Wewe ni uzima, sisi tu wagonjwa, twakujia utuponye
    Tumwendee nani, tukielemewa, kitulizo chetu wewe.
 
5. Na siku ya kufa, utukufu wako, tujaliwe kuuona;
    Milele milele, milele milele, tupumzike kwa amani.

Maoni - Toa Maoni

Reginald Mtimawangu Dec 09, 2018
Nabarikiwa mno na wimbo huu kipindi hiki cha advent. Amina

Lucas Jacob Dec 17, 2017
Kwa kweli wimbo wa karibu bwana njoo naupenda sana, nataka kujua cd yake na dvd ili nipate kuusikiliza

Toa Maoni yako hapa