Mtunzi: Himery Msigwa
> Mfahamu Zaidi Himery Msigwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Himery Msigwa
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 2,948 | Umetazamwa mara 5,776
Download Nota Download MidiKIITIKIO
Ee Bwana utuonyeshe rehema zako (Bwana) utupe rehema zako x 2
MASHAIRI.
1(A) Nanisikie atakavyosema Mungu Bwana maana atawaambia watu wake amani.
(B) Hakika wokovu wake u karibu na wamchao utukufu ukae katika nchi yote.
2(A) Fadhili na kweli zimekutana haki na amani zimebusiana.
(B) Kweli imechipuka katika nchi haki imechungulia kutoka mbinguni
3(A) Naam Bwana atatoa kilicho chema na nchi yetu itatoa mazao yake.
(B) Haki itakwenda mbele zake nayoitazifanya hatua zake kuwa njia.