Mtunzi: Mmole G.
> Tazama Nyimbo nyingine za Mmole G.
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Gereon Mmole
Umepakuliwa mara 1,476 | Umetazamwa mara 3,243
Download Nota Download MidiKiitikio:
Ee Bwana utuonyeshe reehema zako utupe wokovu wako.X2 utupe wokovu wako, wokovu wako, utupe wokovu wako x2
Viimbilizi:
1. Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, maana atawaambia watu wake amani, hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.
2. Fadhili na kweli zimekutana, haki na amani zimebusiana, kweli imechipuka katika nchi, haki imechungulia kutoka mbinguni.
3. Naam, Bwana atatoa kilicho chema, na nchi yetu itatoa mazao yake, haki itakwenda mbele zake,
nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.