Mtunzi: Mmole G.
> Tazama Nyimbo nyingine za Mmole G.
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Gereon Mmole
Umepakuliwa mara 804 | Umetazamwa mara 3,499
Download Nota Download MidiKiitikio:
mkamate elimu, usimwache aende zake, mkamate sana elimu. x2 Mshike maana yeye ni uzima wako, usimwache aende zake mkamate sana elimu. x2
Viimbilizi:
1. Mkamate elimu, usimwache aende zake mshike sana, e limu ni mwanga wa maarifa yote, na busara yake ni adili.
2. Elimu ni paji la Roho Mtakatifu, twajaliwa kuelewa maneno ya ufahamu, elimu yatufundisha matendo ya busara, na kutuongoza katika haki na adili.
3. Elimu huwapa wajinga werevu, na kijana hupata maarifa na hadhari, naye mwenye hekima asikie, na kuongezewa elimu, naye mwenye ufahamu, ayafikie mashauri yenye njia.
4. Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, bali wapumbavu hudharau hekima na adabu, Bali wamchao Bwana na kumkamata elimu, hao wafanyao hayo wana akili njema.