Mtunzi: Daniel Denis
> Mfahamu Zaidi Daniel Denis
> Tazama Nyimbo nyingine za Daniel Denis
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Daniel Denis
Umepakuliwa mara 521 | Umetazamwa mara 1,630
Download Nota Download MidiKiitikio: Ee Mungu Mfalme wangu, nitalitukuza, nitalitukuza jina lako milele.
Mashairi: 1. Ee Mungu wangu Mfalme,nitakutukuza, nitalihimidi jina lako milele, milele na milele
kila siku nitakuhimidi, nitalisifu jina lako milele na milele.
2. Bwana anafadhili ni mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
ni mwingi wa rehema, Bwana ni mwema kwa watu wote, na rehema zi juu ya viumbe
vyake vyote.
3. Ee Bwana viumbe vyako, vyote vitakushukuru, na wacha Mungu wako, watakuhimidi,
watakuhimidi, waunena utukufu wa ufalme wako, na kuuhadidhia uweza wako.
4. Ufalme wako, ni ufalme wa zamani zote, na mamlaka yako yote niya vizazi vyote
huwainua wote walioinamia chini.