Mtunzi: Fr. Gregory F. Kayeta
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Gregory F. Kayeta
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Watakatifu | Shukrani
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 5,469 | Umetazamwa mara 13,179
Download Nota Download MidiEE MUNGU MKUU [Fr. G. F. Kayetta]
//Ee Mungu Mkuu, mwema na Mwenyezi, sifa ni zako, utukufu na heshima; ewe Bwana usifiwe siku zote na viumbe vyako vyote.//
1. Usifiwe, ee Bwana, na Ndugu Jua, ang’ara kwa fahari kutuangaza, na siku zote akutangaza wewe Mkuu.
2. Usifiwe ee Bwana, na Dada Mwezi, na Nyota za angani ulizoweka, Angavu nazo nzuri mno zakusifu wewe.
3. Usifiwe ee Bwana na Ndugu Upepo, na hewa, na mawingu, majira yote. Hivyo wawapa chakula viumbe wako wote
4. Usifiwe Ee Bwana na Dada majii, Usifiwe ee Bwana na Ndugu Moto; Vyote vyatufaa sana, vya thamani kubwa.
5. Usifiwe ee Bwana, na Mama Ardhi, atupaye riziki, na kutulisha, kwa matunda na maua na majani yote.
6. Usifiwe Ee Bwana na wale wote, Ambao husamehe wenzao wote, Na kuvumilia magonjwa na masumbuko.
7. Usifiwe ee Bwana na Dada Mauti, ambaye mwanadamu awaye yote, hawezi kamwe kumuepa Dada huyo.
8. Enyi viumbe vyote mtukuzeni Bwana, Msifuni Bwana wangu, mshukuruni wote, Mtumikieni kwa unyenyekevu mkubwa.