Mtunzi: Fr. Gregory F. Kayeta
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Gregory F. Kayeta
Makundi Nyimbo: Mazishi
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 16,322 | Umetazamwa mara 28,806
Download Nota Download Midi
FR. G.F. KAYETA
MBEYA CATHEDRAL
1. Hapa we msafiri simama na tazama, simama na tazama Nimekufa leo (kesho) ni zamu yako (ona) ona vema nilivyowekwa humu na nilivyo acha mali na jamaa.
2. Nilitoka uchi tumboni mwa mama yangu (Tumboni mwa mamangu) na kurudi uchi (kati)ka tumbo la nchi (sanda) sanda moja hilo ni vazi langu, wameninyang'anya hata senti moja.
3. Nifunike vema na hilo jembe lako (na hilo jembe lako) nilitangatanga (kati)ka ulimwengu (basi) Basi leo kiburi kimekwisha, kumbe dunia hii ni mti mkavu.
4. Nyumba yangu leo ni shimo udongoni (ni shimo udongoni) hakuna mlango (haku)na madirisha (kita) kitanda changu na Blanketi langu, Ni udongo mzito wanielemea.
5. Kifafanuacho watu mbele ya Mungu (watu mbele ya Mungu) si cheo kikubwa (sida)raja sisifa (mate)matendo mema saa ya kufa kwangu, yatafungua mlango wa mbinguni (au) (uwingu).
6. Ole wangu mimi nilifanya ujinga (Nilifanya ujinga) kwa kuambatana (nawa)tu wa dunia (ona) ona leo wote wameniacha, Hasa watu wale niliowapenda.
7. Unaponiona jiwazie mwenyewe (Jiwazie mwenyewe) kufa siku moja (kwa wo)te ni lazima (japo) Sultani japo ni mtumwa, Mungu atamwita ikiwa saa yake.
8. Nimekufa leo nilipona salama (Nilipona salama) nilijishania (mwenye) Afya mwilini (nama) Na mara moja nikaanguka chini; Labda huamini kwamba nalimzima.
9. Yesu msalabani kateswa vikali mno (kateswa vikali mno) kwa kutukomboa (Aka) mwaga damuye (wahu)wahurumie wote wa toharani, Mwanga wa milele uwaangazie.
10. Kwaherini wote kwaherini wapenzi (kwaherini wapenzi) Nimekwenda kwetu (sita)rudi nyumbani (kwahe)rini Baba kwaheri Mama yangu, Mungu akipenda kwake tukutane.