Ingia / Jisajili

EE MUNGU WANGU MFALME NITAKUTUKUZA Zaburi 145

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 625 | Umetazamwa mara 1,662

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Kiitikio: Ee Mungu wangu Mfalmeb nitakutukuza, Ee Mungu wangu Mfalme nitakutukuza, nitalihimidi jina lako milele na milele. 1.Bwana ana fadhili ni mwingi wa huruma si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema. Bwana kweli ni mwema ni mwema kwa watu wote, na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. 2.Bwana kazi zako zote zitakushukuru, na wacha Mungu wako watakuhimidi. wataunena utukufu wa ufalme wako, na kuuhadithia uweza wako. 3. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa