Ingia / Jisajili

Furaha Na Shangwe

Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 1,241 | Umetazamwa mara 4,170

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

FURAHA NA SHANGWE

//:Furaha na shangwe, vigelegele na nyimbo tumwimbie mkombozi wetu amefufuaka://

//:Tuimbe wote (Aleluya) tushangilie (Aleluya aleluya) tucheze ngoma na tufurahie, tuimbe aleluya (aleluya) Bwana Yesu amefufuka://

1. Baada ya Sabato alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, Mariamu na wenzake walikwenda kaburini, kwa mshangao wakakuta kaburi li wazi.

2. Kwa ghafla palikuwa na tetemeko la ardhi, malaika wa Bwana akashuka, akalivingirisha lile jiwe akalikalia, walinzi wa kaburi wakatetemeka kwa hofu.

3. Malaika kawambia ninajua mnayemtafuta Yesu aliyesulubiwa! Hayuko hapa amefufuka kawatangulia Galilaya, huko Galilaya ndiko mtakakomwona.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa