Mtunzi: Thadeo Mluge
> Mfahamu Zaidi Thadeo Mluge
> Tazama Nyimbo nyingine za Thadeo Mluge
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Thadeo Mluge
Umepakuliwa mara 544 | Umetazamwa mara 1,877
Download Nota Download MidiYanini furaha ya kitambo kidogo iletayo karaha ya milele!x2
1. Ndimi Mungu wako niabudu mimi, usitumikie miungu mingine.
Wala usitaje bure Jina langu shika amri zangu asema Bwana.
2. Ishike Sabato ukaitakase ukaache yote kwaajili yangu.
Usijisumbue na mambo mengine bali tafakari matendo yangu.
3. Muheshimu baba naye mama yako ili siku zako ziongezeke.
Usimuhuzunishe jirani yako kwa kutenda mabaya ili ufurahi.
4. Tena usizini wala kutamani ni chukizo kwangu asema Bwana.
Tunza mwili wako hilo ni hekalu humo Roho yangu inatulia.
5. Usiibe mali ya jirani yako ili ufurahi yeye aumie.
Bali uza vyote ulivyonavyo wape wahitaji nawe nifuate
6. Usishuhudie jambo kwa uongo dhidi ya mwingine ili aumie.
Bali sema kweli ukamuokoe akafurahie asema BWANA.
7. Usiitamani mali ya mwingine wala mke wake na chochote chake.
Nitakufurahia nitakupa uzima ukaishi milele kwenye raha yangu