Ingia / Jisajili

Jubilei Ya Jimbo Kahama

Mtunzi: Augustine Rutakolezibwa
> Mfahamu Zaidi Augustine Rutakolezibwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Augustine Rutakolezibwa

Makundi Nyimbo: Anthem

Umepakiwa na: AUGUSTINE RUTAKOLZIBWA

Umepakuliwa mara 789 | Umetazamwa mara 3,419

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mwaka wa Jubilei wa uhai wa jimbo letu Jimbo ni kwetu kahama miaka ishirini na tano,

(Kristu mwanga, Kristu mwanga wa jimbo letu kahama Ni wajibu wetu sote tulipende jimbo letu

Tuone fahari, fahari ya imani yetu ) x2

2. Ee Mungu twashukuru kwa kutufanya kuwa jimbo, tunaona fahari kubwa baraka na heshima.  Makasisi, watawa, walei wote jimboni, nijukumu, letu sote kutunza imani yetu, Tumkubali Kristu, aongoze maisha yetu.

3. Ni miaka mia moja sasa na kumi na saba, tangu wamisionari walipoleta imani, Injili ika s-tawi polepole jimboni, kupitia maombezi ya Mama yetu Maria, Sasa ni jubilei tangu tulipo pata Jimbo.

4. Mwaka moja tisa nane nne jimbo likawepo, tangu tulipoanza viongozi wetu wawili, As-kofu wa_kwanza Mhashamu Shi_ja, Baba Minde ni wa pili katika jimbo Kahama, Kazi wameifanya, kufikia mahali tupo.

5. Ee e Baba tunaomba kwa nguvu ya Roho wako, uamshe mioyo ya waamini wetu wote, Tuitunze, tutetee, imani katoliki, tuiishi, kwa matendo na ujasiri mkubwa, Tuonee fahari, fahari ya imani yetu.

6. Tuimarike zaidi tukiwa jumuiani, kwa_ moyo roho moja tutadumu kwa imani, Kina baba kina mama, enyi kaka na dada, ni wajibu wetu sote tushiriki jumuia, zikawe chemichemi, kuikuza imani yetu.

7 Ee Mungu wa huruma na pia nazo rehema, tunapoadhimisha jubilei yetu ya jimbo, Tunakiri, makosa,tukikuomba toba, tubadili, mienendo, ya maisha mabaya, Tukawe watu wapya, kwa maisha yetu ya mbele


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa