Maneno ya wimbo
Kiitikio:
Leo ni siku ya ta-tu Bwana amefufuka, amemshinda sheta-ni nasi tumekombolewa. {Natuimbe aleluya (Aleluya Aleluya Aleluya Aleluya) natuimbe kwa shangwe Bwana Yesu kafufuka} ×2
Mashairi:
1. Malaika akawaambia msiogope kwa kuwa mnayemtafuta hayupo hapa, amefufuka kama alivyosema.
2. Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma alimtokea kwanza Mariamu Magdalene kupita yeye watu walipashwa habari ya ufufuo wake Mwokozi wetu Yesu Kristo.
3. Kristo ndiye tumaini letu siku zote, leo ni siku ya tatu Bwana kafufuka [atukumbusha kuamini yote tuliyoambiwa na manabii] ×2
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu