Ingia / Jisajili

Kanisa Ni Moja

Mtunzi: John Kasole (Jk)
> Mfahamu Zaidi John Kasole (Jk)
> Tazama Nyimbo nyingine za John Kasole (Jk)

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito

Umepakiwa na: gervis ladislaus

Umepakuliwa mara 683 | Umetazamwa mara 2,316

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Kanisa ni moja alotuachia Bwana wetu Yesu Kristu, Katoliki la kitume.

Ni msingi imara na wa ukweli, hautoyumba milele, kizazi hata kizazi.

Madhehebu ni mengi lakini kanisa ni moja tu, tusidanganywe na manabii waongo tushikirie imani yetu * 2

MABETI

  1. Kanisa ni moja Katholiki la kitume, linaloamini katika MUNGU mmoja, tusitangetange, tusije potea, tushikamane katika imani
  2. Bwana Yesu alisema tushike Imani, imani ya kweli aloacha kwa mitume, tusiyumbeyumbe, kwa kusikiliza maneno ya manabii waongo
  3. Mtiririko wa Ibada zake ni bora, Liturujia yenye upako wa kitume, tuepe maneno yakutuyumbisha, tushikamane katika imani

Maoni - Toa Maoni

Leonard May 21, 2024
Nota za kanisa la katoliki kitabu Cha nota ya liturjia ya kanisa

Toa Maoni yako hapa