Ingia / Jisajili

Karamu Ya Bwana

Mtunzi: Gustav G. Hofi
> Mfahamu Zaidi Gustav G. Hofi
> Tazama Nyimbo nyingine za Gustav G. Hofi

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Gustav Hofi

Umepakuliwa mara 350 | Umetazamwa mara 1,350

Download Nota
Maneno ya wimbo

Kiitikio

Karamu ya Bwana i tayari jongeeni mezani kwa Bwana wateule wanyofu wa moyo Bwana atuita. Haya ndugu jiulize (ndugu) tafakari ndugu jongea mbele kwenye karamu (ya Bwana), ni mwili na damu ya Bwana Yesu Kristu.

Mashairi

1. Upendo wa Yesu ni mkuu sana amejitoa kwa ajili yetu twende tukale chakula cha uzima wetu tupate uzima wa milele.

2. Karibu moyoni mwangu Yesu wangu uishi nami ukanihuishe, uzima mpya wa roho yangu nijalie nipate uzima wa milele.

3. Mwili nayo damu yake Yesu ndio uzima wa roho zetu, Mungu Mwana ungana nasi viumbe wako uondoe udhaifu wetu

Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa