Mtunzi: Deo Kalolela
> Mfahamu Zaidi Deo Kalolela
> Tazama Nyimbo nyingine za Deo Kalolela
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: KASULE JAMES
Umepakuliwa mara 7,448 | Umetazamwa mara 14,920
Download Nota Download MidiKaribu moyoni mwangu leo Yesu wangu mpenzi,
Ukae na mimi siku zote zamaisha yangu.
1. Nikitazama pande zote pande za dunia na waona watuwamea furaha moyoni, namyuso zao zimejaa furaha kamili kwasababu Bwana amewapa furaha kamili.
2. Nami Bwana ninatamani furaha ya kweli, niungane leo na wenzangu nikufurahie, Niupokee mwili wako pia damu yako, nisione njaa wala kiu siku zangu zote.
3. Ninakuja sasa ee Bwana kwa furaha kubwa,nipokee Bwana yesu wangu nifurahi nawe,
Mzigo mzito wa dhambi siutki tena, ninakukabidhi moyo wangu pia mwili wangu.