Mtunzi: Felician Albert Nyundo
> Tazama Nyimbo nyingine za Felician Albert Nyundo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Gervas Kombo
Umepakuliwa mara 1,298 | Umetazamwa mara 5,104
Download Nota Download MidiMfalme wa mbinguni karibu njoo uje mioyoni karibu njoo ukae nasi karibu njoo
1. Ewe Yesu mfalme, karibu njoo,
Uje unilishe, karibu njoo,
Na uninyweshe karibu njoo.
2. Utuimarishe, karibu njoo,
Na ututulize, karibu njoo,
Tufarijike, karibu njoo.
3. Njoo utusafishe, karibu njoo,
Roho zitakate, karibu njoo,
Utuokoe, karibu njoo.
4.Utuangazie, karibu njoo,
Mbingu tuione, karibu njoo,
Utuongoze, karibu njoo