Mtunzi: Alvin Marie
> Mfahamu Zaidi Alvin Marie
> Tazama Nyimbo nyingine za Alvin Marie
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Alvin Marie
Umepakuliwa mara 1 | Umetazamwa mara 0
Download Nota Download MidiKila kipaji kilicho chema, na zawadi kamili, vyote hutoka juu mbinguni kwa Baba wa mianga x2 Basi ni nani aijuaye nia ya Mungu? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Tena ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, ili akalipwe tena? Vitu vyote vyatoka kwake, navyo vipo kwa uweza wake; tena vyote vinarejea kwake.
1. Tusidanganyike na kufikiri kuwa ni mali zetu, kwa kuwa vyote ni vya Mungu.
2. Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya Mungu, hakika vyote ni vya Mungu.
3. Kwa sura na kwa mfano wa Mungu tazama tumeumbwa, na sisi pia ni wa Mungu