Mtunzi: Chris Oyier
> Mfahamu Zaidi Chris Oyier
> Tazama Nyimbo nyingine za Chris Oyier
Makundi Nyimbo: Tenzi za Kiswahili
Umepakiwa na: CHRIS OYIER
Umepakuliwa mara 732 | Umetazamwa mara 2,543
Download Nota
KIOO NI YESU - Na Chris Oyier
Nimefunuliwa jambo moja, jambo hilo waziwazi.
Lipi, kipi, wapi, jambo hilo, jambo hilo ni kioo.
(Kioo, kioo, kioo, kioo, kioo) Kioo huyu ni Yesu. (Je wajua Yesu ni kioo) tega sikio ujue. >>>>
1. Yesu kazaliwa Bethlehemu horini mwa ng'ombe, kawacha ufalme wake, kaunganika na udhaifu , wa mwanadamu, mateso hapa duniani.
(Kwa hivyo), kioo ni kuunganika na wale wasojiweza, wape matumaini, na kuwasaidia.
2. Mfalme Herode kwa hofu alipanga kumuua Yesu, Malaika akatumwa, kamwambia Yosefu torosha, Maria na Yesu, wasidhurike na Herode.
(Kwa hivyo) kioo ni kuisikia sauti ya Mungu wetu, kumuamini yeye, kuwa atulinda vyema.
3. Yesu kafunga jangwani shetani kamjaribu, akamshinda shetani, kwa nguvu za Mungu Baba yake, akapata roho, kufa kwa dhambi zetu.
(Kwa hivyo) kioo ni kumtumaini Mungu atupe nguvu, kushinda majaribu, na maovu ya dunia.
4. Yesu kafanya miujiza kahubiria watu, kaonesha mfano bora, kwake kusali kila wakati, kuwa mtumishi, kukomboa wanadamu.
(Kwa hivyo) kioo ni kusali kila wakati bila kukoma, sote kujitolea, kufanya kazi ya Mungu.
5. Yesu alikataliwa na akasulibiwa, kwa makosa yetu sisi, akafa na pia kafufuka, kashinda mauti, katukomboa dhambini.
(Kwa hivyo ) kioo ni kuvumilia mateso na kusimangwa, mwisho tavikwa taji, ya uzima wa milele.