Mtunzi: Chris Oyier
> Mfahamu Zaidi Chris Oyier
> Tazama Nyimbo nyingine za Chris Oyier
Makundi Nyimbo: Watakatifu
Umepakiwa na: CHRIS OYIER
Umepakuliwa mara 332 | Umetazamwa mara 1,796
Download Nota Download Midi
MBARIKIWA YOSEFU ALLAMANO UTUOMBEE
1.
Mbarikiwa Yosefu Allamano, uliye somo wetu, tunakusihi, utuombee kwa Mungu Baba.
Katika safari yetu ya utakatifu, utuombee sisi, tuweze kufuata njia kutufikisha kwa Mungu.
Tuwe Watakatifu kabla kuwa Wamishonari, tuwe Watakatifu kabla kuwa wanakwaya, tuwe Watakatifu kabla kuwa viongozi wa kanisa, ulitufunza, kuwa utakatifu huja, kabla kuwasaidia wengine kuwa watakatifu. Huwezi kupeana kile ambacho huna.
2.
Mbarikiwa Yosefu Allamano, uliye somo wetu, tunakusihi, utuombee kwa Mungu Baba.
Katika safari yetu ya utakatifu, utuombee sisi, tuweze kufuata njia kutufikisha kwa Mungu.
Nyoyo zetu zitaokolewa kwa utakatifu, sote tuokolewe mwisho tumuone Mungu, maishani tufanye kila kitu vyema pia iwe siri, ulitufunza, tumuige Mungu kwa yote, tutakuwa tumeishi maisha ya utakatifu, maisha yetu yawe funzo, utakatifu.
3.
Mbarikiwa Yosefu Allamano, uliye somo wetu, tunakusihi, utuombee kwa Mungu Baba.
Katika safari yetu ya utakatifu, utuombee sisi, tuweze kufuata njia kutufikisha kwa Mungu.
Ulivyomsikiza Mama wa Consolata mkaanzisha, shirika la kimishonari la Consolata, tufanye kazi pamoja kueneza injili yake Mungu, ulitufunza, hekima huja kwa shauri, ushauri ni umoja kufanya kazi yake Mungu. Tushirikiane katika kazi ya Mungu.