Maneno ya wimbo
Kiitikio: Kwako Bwana Mungu Kwako zinatoka sifa zangu kwako zinatoka sifa zangu katika kusanyiko kubwa katika kusanyiko kubwa.
1. Nitaziondoa nadhiri zangu mbele yao wamchao wapole watakula na kushiba, wamtafutao Bwana watamsifu mioyo yenu na iishe milele.
2.Miisho yote ya dunia itakumbuka, na watu watakurejea, jamaa zote na mataifa watamsujudia, wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, humwinamia wote washukao mavumbini.
3. Naam yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake, wazao wake watamtumikia. zitasimuliwa habari za Bwana kwa kizazi kitakachokuja, nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake, ya kwamba ndiye aliyefanya.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu