Ingia / Jisajili

Kwako Bwana

Mtunzi: John Mgandu
> Tazama Nyimbo nyingine za John Mgandu

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 7,167 | Umetazamwa mara 14,578

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kwako Bwana zinatoka sifa zangu sifa zangu kwako Bwana zinatoka sifa zangu x 2
Katika kusanyiko, katika kusanyiko kusanyiko kubwa Aleluya (Aleluya) Aleluya x 2

  1. Nitaziondoa nadhiri zangu, mbele yao wamchao, mbele yao wamchao, wapole watakula na kushiba, wamtafutao Bwana watamsifu.
     
  2. Miisho yote ya dunia itakumbukwa na watu watamrejea Bwana na watu watamrejea Bwana jamaa zote za mataifa watamsujudia, wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu.
     
  3. Zitasimuliwa habari za Bwana kwa kizazi kitakachokuja, kwa kizazi kitakachokuja, nao watawahubiri watakaozaliwa haki yake, ya kwamba ndiye aliyefanya, ndiye aliyefanya.

Maoni - Toa Maoni

Peter paul Apr 27, 2018
Hongera sana wimbo safi

Toa Maoni yako hapa