Ingia / Jisajili

Nirudieni Mimi

Mtunzi: Aloyce Goden Kipangula
> Tazama Nyimbo nyingine za Aloyce Goden Kipangula

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 50,550 | Umetazamwa mara 94,928

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Lakini hata sasa asema Bwana nirudieni, mimi kwa mioyo yenu yote x 2

Mashairi:

1. Fanyeni mabadiliko mioyoni mwenu, kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza - nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote.

2. Pigeni Tarumbeta huko Sayuni, waambieni watu wote ili wafunge - nirudieni mimi...

3. Kusanyeni watu wote waleteni kwangu, waleteni na watoto hata wazee - nirudieni mimi ...

4. Mpingeni yule mwovu atawakimbia, nikaribieni nami nitawakaribia - nirudieni mimi ...

5. Takaseni mikono yenu iliyojaa dhambi, safisheni mioyo yenu yenye nia mbili - nirudieni mimi ...


Maoni - Toa Maoni

Tavisama Ushindi Aristote Apr 07, 2022
Mungu ni mwema kwa wote

Kahindi Misigah Jan 16, 2022
Wimbo mzuri na umepangwa vizuri. Iko shida kudownload MIDI

Renatus Mfilinge Mar 20, 2021
Hongereni kwa wimbo huu mtamu. Umenibariki sana na huwa naupenda sana!

Desdery Pius Mwase Sep 03, 2018
NASHUKURU KWA WIMBO MZURU,PONGEZI KWA MTU WA WIMBO PIA KWA WANAKWAYA WOTE...NA KUANZIA SASA NABADILIKA KWELI KIROHO NA KIMWILI ..MWENYENZI MUNGU NISAIDIE MIMI PIA NA WENGINE TULIOAMUA KUACHA DHAMBI NA KUTENDA YALE YANAYOENDANA NA MAPENZI YAKO .AMINA

Francisco Charles Mar 01, 2018
Ipo vizur sana hongereni

Stephen Moshy Feb 14, 2018
Nasikitika kwa kutoijua hii web mapema. nimeipenda sana

Saraphina Jan 03, 2018
Ubarikiwe uliyetunga wimbo huu huwa nabarikiwa sana.

Ambrose msella Mar 29, 2017
Wimbo uko vzr sana ila nikitaka kudownload inashindikana nifanyaje?

Michael Nzuki Makiti Mar 24, 2017
Nawapongeza waimbaji wenzanzu! Bwana awabariki sana, nyimbo zenu zote nizamaajabu, sauti tamu kabisa

paschal evarst Mar 13, 2017
Pongeza, kwa kazi nzuri Kosoa.... Uwe mstaarabu

Grace Mwaya Mar 06, 2017
Hongereni sana Chang'ombe choir singers. Wimbo ni nzuri unanibariki sana. Mbarikiwe sana na muendelee kuinjilisha kwa njia ya nyimbo.

LEONARD Nov 23, 2016
NAPENDA KWAYA

kadam lwenje Nov 20, 2016
hongera sana nitaupataje

michael julius Oct 28, 2016
jina la wimbo lina itwaje

Bruno Protasi Sep 10, 2016
Pongeza Wimbo Mzuri Sana Mungu Akupe Maujuzi Zaidi

benito adam Aug 24, 2016
Pongeza, Kosoa.... Uwe mstaarabu

thompson shuma Jul 22, 2016
wimbo mzuri unahiti vizuri hongera sana tunasubiri video kama inakuja

Toa Maoni yako hapa