Maisha mvuke by A.H Gonzaga (3/4- B flat)-SPNC
Leo nipo hapa ila ya kesho sijui, kwa maana maisha haya ni kama mvuke.
Yaonekana, mara yatoweka. Nifunze Bwana kuzihesabu siku. Na nitamweka Kristo moyoni, yeye ni mwamba wangu daima.
Maisha haya ni kama mvuke, hayadumu yapita kwa haraka. X2
Ninayo mawazo mengi nitakavyoishi, nauliza sababu gani niumbwe mimi.
Lakini kweli lipo tumaini, kwa sababu namtazamia Yesu. Lakini kweli lipo tumaini, maana yeye yupo nami hakika.
Hitimisho (C major)
Ee Roho Mtakatifu uniongoze, sitaogopa chochote nikiwa nawe. (Matatizo ya kila siku nitakumbana nayo. Hata mvuke ukiisha, ninaye Yesu. X2)