Mtunzi: Gerald Cuthbert
> Mfahamu Zaidi Gerald Cuthbert
> Tazama Nyimbo nyingine za Gerald Cuthbert
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Ndoa | Shukrani
Umepakiwa na: Gerald Cuthbert
Umepakuliwa mara 391 | Umetazamwa mara 1,262
Download Nota Download MidiMashairi:
1. Nikikumbuka Maisha niliyopitia, Toka nizaliwe yananiumiza Mungu wangu,Ni maisha ya shida na tabu ndani yangu, leo moyo wangu waimba neema zake Mungu.
Chorus:
Ni Neema zake Mungu (na) ni Neema zake, Si mimi sio nguvu zangu ni Neema zake Mungu.Ni Neema zake Mungu (na) ni Neema zake, Si mimi sio nguvu zangu ni Neema zake!
2. Ee Mungu wangu unihurumie mimi sasa, Wewe uliyeniumba mimi pasipo kujua,Unikomboe mimi nilipopotea, Ninapoanguka naamini wewe huniachi.
3. Na dunia hii sio yetu Bwana Mungu, Sasa nakuomba ziangazie hatua zanguNa roho yangu roho iliyopondeka, Uiepushie maovu ya humu duniani.
4. Haya maisha bila yesu mimi ni bure, Nimejaribu tena ni mengi yameshindikana,We anza naye katika unalofanya,Maliza na yeye utaona Neema za Mungu.