Ingia / Jisajili

Mali Yako

Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 6,778 | Umetazamwa mara 13,232

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Utangulizi:

Mali yako Mali Yako, Mali yako, na vinatoka kwako vyote mali yako na vinatoka kwako
Mkate wetu nayo divai yetu Dhabihu zetu nayo divai yetu mali yako mali yako mali yako

 1. Mali yako nguvu zangu na uhai wangu familia na jamii yangu Fedha nilizonazo ni zako mazao nivunayo ni yako

  Kiitikio
  (Organ) Milele (Organ) Mi (Organ) Mi (Organ) Milele (Utukuzwe utukuzwe Bwana Mungu milele) x 2Maana kwa wema wako tumepokea huu mkate na kutoka kwako tumepokea hii divai.


 2. Mali yako:Umri wangu na ujana wangu
  Shida zangu furaha zangu
  Na vipaji vyangu vyote x2(KIITIKIO)

 3. Mali yako:Ndoa yangu na uchumba wangu
  Utume ukasisi na utawa wangu
  Mwili na roho yangu ni vyako x2(KIITIKIO)

 4. Mali yako:Utajiri na elimu yangu
  Umaarufu wangu mkubwa
  Hadhi niliyo nayo ni yako,
  Unyonge wangu pia ni wako (KIITIKIO)

 5. Mali yako:Nifanye kazi kwa ushujaa
  Niipe jamii manufaa
  Nimalize nitoke upesi
  Nirudi kulekuliko kwako (KIITIKIO)


Maoni - Toa Maoni

Thomas Jun 06, 2017
Ninapenda music

Toa Maoni yako hapa