Mtunzi: Yudathadei Chitopela
> Mfahamu Zaidi Yudathadei Chitopela
> Tazama Nyimbo nyingine za Yudathadei Chitopela
Makundi Nyimbo: Epifania
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 2,858 | Umetazamwa mara 6,525
Download Nota Download MidiKIITIKIO:
Mataifa yote ya ulimwengu watakusujudia Ee Mungu,
Mataifa yote ya ulimwengu watakusujudia Ee Mungu
MASHAIRI:
1.Ee Mungu mpe Mfalme hukumu zako, Na mwana wa Mfalme haki yako,
Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
2.Siku zake yeye Mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma,
Na awena enzi toka Bahari hata Bahari, Toka mto hata miisho ya dunia.
3.Wafalme wa Tarshishi na visiwa walete kodi, Wafalme wa sheba na seba watoe vipawa,
Naam Wafalme wote na wamsujudie, Na Mataifa yote wa mtumikie.
4.Kwa maana atamwokoa mhitaji aliapo, Na mtu aliyeonewa iwapohana msaidizi,
Ata mhurumia aliye dhaifu na masikini, Na nafsi za wahitaji ataziokoa.