Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Vusile Silonda
Umepakuliwa mara 20,457 | Umetazamwa mara 28,206
Download Nota Download MidiHiki kidogo, kikakupendeze, ni matoleo ya wana wako x 2
1. Mkate divai madhabahuni, ni matoleo ya wana wako
Malimbuko ya juhudi zetu, ni matoleo ya wana wako
2. Fedha tulizotolea jasho, ni matoleo ya wana wako
Ziwe ishara ya nia zetu, ni matoleo ya wana wako
3. Sala maombi shukrani, ni matoleo ya wana wako
Na nyimbo zetu zipae kwako, ni matoleo ya wana wako
4. Tukutukuze katika yote, ni matoleo ya wana wako
Uhimidiwe milele yote, ni matoleo ya wana wako