Mtunzi: Benny Weisiko John
> Mfahamu Zaidi Benny Weisiko John
> Tazama Nyimbo nyingine za Benny Weisiko John
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Benny Weisiko
Umepakuliwa mara 1,020 | Umetazamwa mara 3,642
Download Nota Download Midichorus
Mimi na nyumba yangu (mimi) nitakutumikia Mungu x2
nisali niimbe (tena) shangwe nikae mikononi mwako (kwa kuwa)
uhai wangu na mali zangu vyote vinatoka kwako (kwako Mungu wangu) nisali niimbe (tena) kwa shangwe nikae mikononi mwako
(kwa kuwa) uhai wangu na mali zangu vyote vinatoka kwako.
1.Hakika Mungu wewe wanijalia neema nyingi, na hivyo Bwana naimba kwa nyimbo nzuri nikisifu jina lako.
2.Nikupe nini Bwana kilingane na fadhili zako, tazama sina ila nakurudishia sifa ewe Mungu wangu.
3.Unipe nguvu mimi nimshinde shetani muovu, na mwisho nami nifike juu mbinguni Bwana nikutumikie.