Ingia / Jisajili

Mshukuruni Mungu

Mtunzi: Noel S.Munyetti
> Mfahamu Zaidi Noel S.Munyetti
> Tazama Nyimbo nyingine za Noel S.Munyetti

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Noel Seni Munyetti

Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ninayo kila sababu ya kumshukuru Mungu, kwa kuwa amenitendea mema mengi.

Nitaimba sifa zake Mungu aliye Muumba wangu, wema wake Mungu kwangu ni wa ajabu.

(Mshukuruni Bwana Mungu wetu mwenye nguvu na Enzi.

Tumwimbieni Mungu nyimbo nzuri tumwambie twashukuru)×2

1. Umeweka nyimbo za kushukuru kinywani mwangu, na siku zote nitasimama na kushuhudia kuwa upendo wako hauna mwisho na huruma zako hazina mipaka.

2. Kwa hapa uliponifikisha nina mengi ya kueleza. Tangu kuzaliwa kwangu hakika ni wewe.

3. Wewe uliye sikia sauti ya dua zangu, Hukuruhusu adui zangu wanicheke, uligeuza machozi kuwa kicheko kwangu, Hakika wewe Bwana ni mwema.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa