Ingia / Jisajili

Msingi Wa Ukombozi Wetu Umeshajengwa (Krismasi)

Mtunzi: Robert A. Maneno (Aka Albert)
> Mfahamu Zaidi Robert A. Maneno (Aka Albert)
> Tazama Nyimbo nyingine za Robert A. Maneno (Aka Albert)

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Albert Maneno

Umepakuliwa mara 152 | Umetazamwa mara 3,526

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Msingi wa Ukombozi wetu Umekwisha jengwa, Bwana Yesu Mkombozi amezaliwa huko Bethlehemu.

Kazaliwa mtoto ndiye Kristo Bwana na Mkombozi wetu.

1.Tazama Bikira alichukua mimba na leo imetimia Mtoto kazaliwa,huyo mtoto ameitwa Imanueli kama ilivyo agizwa na Malaika.

2.Tazama tumeona nyota yake mashariki.Yu wapi mtoto mfalme aliyezaliwa? Hayo yote yalinenwa na Mamajusi walofika kumsalimu Mtoto Yesu.

3. Herode kataharuki kusikia hayo. Ka'ita wakuu wa Makuhani kuwauliza.Wakamjibu Kristo azaliwa Betlehemu ma'na ndivyo ilivyoandikwa na Nabii.

4. Betlehemu nchi ya Yuda,hu'mdogo kamwe, Kwa kuwa kwako atatoka mtawala, atachunga watu wangu I sraeli, atakaye wachunga watu wangu Israeli

(Rejea Mt. 1: 18 - 23; Mt. 2: 1 - 7


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa