Mtunzi: Mmole G.
> Tazama Nyimbo nyingine za Mmole G.
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Gereon Mmole
Umepakuliwa mara 983 | Umetazamwa mara 3,418
Download Nota Download MidiKiitikio:
Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana. [Mwiteni (mwiteni) maadamu yu karibu mwiteni (mwiteni) maadamu yu karibu, mwiteni (mwiteni) mwiteni, maadamu yu karibu.] x2
Viimbilizi:
1.Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake, na amrudie Bwana naye atamsamehe, na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa.
2.Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana.
3.Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.