Ingia / Jisajili

Mungu kwa mema yako yote asante

Mtunzi: Pancras Shayo Justine (Mzungu Jp)
> Mfahamu Zaidi Pancras Shayo Justine (Mzungu Jp)
> Tazama Nyimbo nyingine za Pancras Shayo Justine (Mzungu Jp)

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Pancras Justine

Umepakuliwa mara 366 | Umetazamwa mara 1,221

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
KIITIKIO: Twakushukuru Ee Mungu kwa mema yako [yote] uliyotujalia twasema asante, asante Mungu wetu fanaka tulizonazo ni wema na ukarimu wako; mastahili yetu yangefaa nini[kweli] kwa mema unayotujalia! VIIMBILIZI: 1. Umetulisha umetunywesha, kwa Mwili na Damu yako Takatifu Asante, asante Mungu wetu. 2. Watulinda sisi na ajali mbaya, watukinga nayo maradhi mabaya Asante, asante Mungu wetu. 3. Tukitenda kazi watufanikisha, tukielemewa watupumzisha Asante, asante Mungu wetu. 4. Upokee Baba shukrani zetu kwa njia ya Kristo Bwana Mungu wetu Asante, asante Mungu wetu.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa