Maneno ya wimbo
Kiitikio:
Mungu Mungu unihifadhi mimi x2 kwa maana nakukimbilia wewe nakukimbilia wewe nakukimbilia wewe x2
Maimbilizi:
1.Mungu unihifadhi mimi kwa maana nakukimbilia wewe, nimemwambia Bwana ndiwe Bwana wangu, Bwana ndiye fungu la posho langu.
2.Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri naam, mtima wangu umenifundisha usiku, nimemweka Bwana mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa.
3.Kwa hiyo moyo wangu unafurahi na utukufu wangu unashangilia naam, mwili wangu utakaa kwa kutumaini, maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
4.Utanijulisha njia ya uzima, mbele ya uso wako ziko furaha tele, na katika mkono wako wa kuume, mna mema mna mema ya milele.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu