Mtunzi: Wickriff Mutwiri
> Mfahamu Zaidi Wickriff Mutwiri
> Tazama Nyimbo nyingine za Wickriff Mutwiri
Makundi Nyimbo: Mwanzo | Shukrani
Umepakiwa na: Wickriff Munene
Umepakuliwa mara 943 | Umetazamwa mara 3,162
Download Nota Download Midi1.(Mwimbieni Bwana nyimbo za shangwe, inueni na la Mungu
wetu)*2
kiitikio
Kwa zaburi pia nyimbo mpya, tangazeni sifa zake kwote,
mwambieni Bwana matendo Yako yatisha kama nini.
Kwa vinanda ngoma vuvuzera, kwa kayamba vinubi na zeze,
tangazeni matendo yake Mungu kwa mataifa yote.
2.(Pigeni kelele pia vifijo,mshukuruni Mungu kwa wema Wake)*2
3.njoni wote wazee kwa viana, tumshukuru Mungu kwa ukarimu
wake
Kusanyikeni mlio hai, tumwimbie Mungu kwa miujiza yake
4.Maaskofu Mapadre na watawa, mshukuruni Mungu kwa Ibada
takatifu
Mtoleni sadaka ya shukrani, iliyoandamwa na moshi wa ubani
Kimalizio.
Wanakwaya na waumini wote eeh, tumwimbie na tumfanyie
shangwe leo
Wazee, vijana pia watoto eeh,Mpigieni kelele za kumsifu leo