Ingia / Jisajili

Niliwapenda Sana

Mtunzi: Wickriff Mutwiri
> Mfahamu Zaidi Wickriff Mutwiri
> Tazama Nyimbo nyingine za Wickriff Mutwiri

Makundi Nyimbo: Mazishi

Umepakiwa na: Wickriff Munene

Umepakuliwa mara 325 | Umetazamwa mara 1,293

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Maneno ya kiitikio

Kwa hakika niliwapenda sana, ila Mungu akanipenda zaidi

Niliowa’cha poleni poleni sana, ahe poleni poleni sana

Msilie wala msitie shaka, nimeenda mbinguni kwa Mungu Muumba

Furahini wala msihuzunike, (siku moja mtakua nami tena)*2

Maneno ya mashairi

1.Mungu Baba ndiye aliyekuumba, vivyo hivyo ndiye Amekuchukua, Penzi Lake Mungu na litimilike

2.Twaiombea roho yako kwake Mungu, Ailaze mahali pema peponi, Alazapo nyoyo za watakatifu

3.Binadamu tuliumbwa kwa mavumbi, Humo humo Mavumbini tutarudi, Hiyo ndiyo hatima yetu sote


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa