Ingia / Jisajili

Mwokozi Amezaliwa.

Mtunzi: Felician P. Bukene
> Tazama Nyimbo nyingine za Felician P. Bukene

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Emmanuel J. R. Nyambo

Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
  • MWOKOZI AMEZALIWA.
  • Ni shangwe leo, ni shangwe leo, ni shangwe leo, Mwokozi amezaliwa.x2

    • Twende Bethlehemu tukamwone mtoto (leo), Yupo na Mamae na Baba Yosefu [(twende na) zawadi, (zawadi) zetu zawadi (sisi) zetu tumpelekee mtoto aliyezaliwa leo.]x2

  • Mashairi:-
  • 1. a/ Mwokozi Yesu kazaliwa, mbinguni kote ni furaha,
  • b/ Maandiko ya manabii, kweli leo yametimia
  • Hongera (Maria) hongera (Yosefu) tufurahi (sote) kwa shangwe kuu.

  • 2. a/ Malaika anawapasha, wachungaji habari njema,
  • b/ Nao wanakwenda haraka, pamoja na zawadi zao,
  • Twendeni (na sisi) haraka (haraka) yukamwone sote mtoto Yesu. 

  • 3. a/ Mama Jusi wanashangaa, kuona nyota ya ajabu,
  • b/ Ndivyo Mungu alivyopenda, kuwapa taarifa njema,
  • Waenda (haraka) kuona ( ni nini) wanabeba wote zawadi nzuri.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa